1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chadema kuwachagua viongozi wa juu

21 Januari 2025

Wagombea wa nafasi ya uenyekiti katika chama kikuu cha upinzani Tanzania Chadema, wameapa kuungana na kuimarisha chama hicho, licha ya matokeo yoyote ya uchaguzi unaofanyika baadae hii leo.

Chadema
Chadema kuwachagua viongozi wa juuPicha: Ericky Boniphace/DW

Mwenyekiti anayemaliza muda wake Freeman Mbowe, na Tundu Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti-Tanzania bara wamesema hii leo kwamba ni muhimu kwao kuendeleza mshikamano na kukijenga chama, bila kujali nani atachaguliwa kuwa mwenyekiti mpya. 

Chadema yakamilisha hatua ya kwanza ya uchaguzi wa mabaraza

Akizungumza na wajumbe wa mkutano wa chama hicho unaofanyika katika jiji la kibiashara la Dar es salaam, Mbowe amesisitiza umuhimu wa umoja na nidhamu ndani ya Chadema, akitoa rai kwa wanachama kujizuia na matusi na migogoro ya ndani.

Kwa upande wake Lissu, ameahidi kujitolea kwake katika kukiimarisha chama bila kujali matokeo ya uchaguzi huo wa uongozi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW