1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CHADEMA waandamana Dar es Salaam

24 Januari 2024

Wafuasi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamefanya maandamano makubwa kwenye mji mkuu wa kiuchumi, Dar es Salaam, wakiongozwa na mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.

Tanzania, Dar es Salaam | Maandamano
Viongozi wa CHADEMA wakiongoza maandamano ya amani jijini Dar es Salaam kudai katiba mpya siku ya Jumatano (23 Januari 2024).Picha: Florence Majani/DW

Maandamano hayo ni ya kuishikiniza serikali kuondoa bungeni miswada mitatu ya mabadiliko ya sheria za uchaguzi na kuboresha katiba mpya, pamoja na mambo mengine.  

Mbowe, pamoja na viongozi wengine wa CHADEMA, Godbless Lema, Benson Kigaila na Joseph Mbilinyi waliongoza msafara wa waandamanaji hao waliokuwa wameshika bendera za chama hicho na mabango yenye jumbe mbalimbali.

Jeshi la polisi lilitoa kibali cha kuwaruhusu kufanya maandamano hayo na kuahidi kuyasimamia.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya mji wa Dar es Salaam, Jumanne Muliro, alifika eneo la Buguruni mapema asubuhi na kuanza kuongoza misafara ya pikipiki na magari kabla ya maandamano hayo kuanza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW