CHADEMA yaenguliwa katika uchaguzi mkuu wa Oktoba
13 Aprili 2025
Mkurugenzi wa uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi NEC Ramadhani Kailima amesema bila ya kukitaja chama kwamba, chama chochote ambacho hakijasaini kanuni hizo hakitaruhusiwa kushiriki katika uchaguzi mkuu au uchaguzi mwingine wowote kwa kipindi cha miaka mitano ijayo na kusisitiza kuwa hakutakuwa na nafasi ya pili.
Hapo jana Jumamosi Katibu Mkuu wa CHADEMA John mnyika alisema hatashiriki katika mkutano wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi INEC, ambao ulilenga vyama vya siasa kusaini kanuni za maadili ya uchaguzi zilizowekwa na serikali.
Soma pia:CHADEMA: Vuguvugu letu ni la kutaka mageuzi sio uhaini
Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, ambaye alikamatwa na kushtakiwa kwa uhaini mapema wiki hii, awali alisema kuwa chama hicho hakitashiriki katika uchaguzi bila ya kuwepo mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi.