1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CHADEMA yatangaza kutosusia uchaguzi mkuu wa Tanzania

12 Februari 2025

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzani Tanzania, CHADEMA, Tundu Lissu amesema chama hicho hakitasusia uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu na badala yake kinakwenda kuhakikisha uchaguzi huo hautafanyika kabisa.

Tanzania | Siasa |  Tundu Lissu
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu LissuPicha: Emmanuel Herman/REUTERS

Akihutubia taifa leo amesema, CHADEMA kitaishtaki serikali ya Tanzania kwa wananchi, jumuiya za kimataifa na viongozi wa kidini ili kuhamasisha mabadiliko ya katiba na sheria za uchaguzi zinazochagiza mifumo mibaya ya uchaguzi inayovunja demokrasia.

Lissu aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa chama hicho Januari 22 amesema mifumo ya uchaguzi Tanzania inadhibitiwa na Rais wa nchi na kwa upande wa Zanzibar pia ukidhibitiwa na Rais.

Soma pia:Chadema yakamilisha hatua ya kwanza ya uchaguzi wa mabaraza
 
Amesema mfumo huo wa uchaguzi wa Tanzania ulisababisha Tanzania kuongozwa na viongozi ambao hawakupigiwa kura kati ya mwaka 2019/2020. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW