Chalsea yatoka sare na Juventus Champions League
20 Septemba 2012Kiungo wa kati wa wa Chelsea Mbrazili Oscar ndiye aliyeipatia klabu yake mabao yote mawili. Ikiwa ni mara yake ya kwanza kabisa kwao kijana huyo mwenye umri wa miaka 21 kushiriki ligi hiyo, Oscar aliwaonyesha mashabiki kwa nini Chelsea iliamua kupoteza kitita cha paundi za Uingereza milioni 25 kumsajili kwa kushinda mara mbili katika dakika tatu za mwanzo dimbani Stamford Brigde.
Sare hiyo ya bao 2-2 iimewanyima raha mabingwa hao watetezi ambapo kocha wake Roberto Di Matteo amesema kuwa wamekosa fursa ya kuanza na ushindi. "Tumevunjika moyo na matokeo haya na kwa kiasi fulani tunajihisi kushindwa. Tulikuwa kwenye nafasi nzuri ya kutoka na ushindi lakini matokeo yake tumeambulia sare tu" anasema Di Matteo.
Kwa upande wao Juventus waliweza kuwanyanyua mashabiki wao vitini dakika 10 baada ya kuingizwa uwanjani Fabio Quagliarella ambaye aliipatia bao la pili timu hiyo.
Nayo klabu ya soka ya Barcelona ya Uhispania imeweza kuonyesha ubabe dhidi ya Spartak Moscow baada ya kuipa kipigo cha bao 3-2. Shukrani za pekee zinakwenda kwake Lionel Mersi ambaye alionyesha juhudi kubwa na kufanikiwa kuipatia ushindi timu yake. Barcelona ndiyo kinara katika kundi G.
Bayern yaanza kwa ushindi
Kwa upande wa klabu ya Bayern Munich kutoka hapa Ujerumani mambo hayakuwa mabaya kwani imeweza kuibuka na ushindi dhidi ya Valencia katika mchezo wake wa kwanza wa taji hilo tangu iliposambaratishwa na Chelsea katika fainali zilizopita mwezi Mei mwaka huu kwenye uwanja wake wa nyumbani.
Manchester United wana wa Sir Alex Ferguson wakiwa katika kundi H ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Galatasaray. ushindi huo unatajwa kama wa kichovu kwani Galatasaray ilionyesha mchezo ambao uliwatoa jasho watoto wa jijini Manchester.
Hata hivyo Sir Alex Ferguson aliaambia wale wanaoona ushindi huo ni mwembamba kuwa kuanza msimu kwa pointi tatu ndilo jambo la msingi kwao hasa ukizingatia kilichowapata mwanzoni mwa msimu uliopita.
Gerard Piques kupata mtoto
Baada ya kujua yanayoendelea katika mbio za kuwania taji la Champion sasa tuangalie mambo yanavyokwenda katika maisha ya mastaa wa kabumbu duniani. Mwanamuziki maarufu wa miondoko ya Pop kutoka Colombia, Shakira ametangaza kuwa na ujauzito wa mchezaji wa kimataifa kutoka Uhispania Gerard Piques.
Kimwana huyo wa Hips Dont lie amesema hiyo ni hatua muhimu na ya pkee katika ulimwengu wa mapenzi baina yake na Gerard na atasimamisha baadhi ya maonyesha kwa wiki kadhaa ili kujipa nafasi ya kupumzika. Huyo atakuwa mtoto wa knza kati ya wenza hao ambao Shakira ana miaka 35 na Gerard ambaye ni mchezaji wa klabu ya kandanda ya Barcelona ana miaka 25 ambao waliweka wazi mapenzi yao mwezi Machi mwaka huu.
Mwandishi: Stumai George/Reuters/AFP