1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha AfD chaongoza katika utafiti wa kitaifa wa YouGov

17 Septemba 2025

Chama cha mrengo wa kulia cha Alternative for Germany (AfD) kimeupiku muungano wa vyama ndugu vya kihafidhina vya CDU/CSU katika kura ya maoni ya shirika la utafiti la YouGov iliyotolewa leo.

Kiongozi wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Mbadala kwa Ujerumani - AFD,  Alice Weidel akiwa katika mahojiano mjini Berlin mnamo Julai 10, 2025
Kiongozi wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Mbadala kwa Ujerumani - AFD, Alice WeidelPicha: Bernd Elmenthaler/ESDES.Pictures/IMAGO

AfD ilipata asilimia mbili zaidi ya pointi ikilinganishwa na utafiti wa mwezi Agosti, na kuongeza umaarufu wake hadi 27%, huku muungano huo wa CDU/CSU ukishuka kwa pointi moja hadi 26%.

Kulingana na utafiti huo wa youGov, ikiwa uchaguzi mkuu ungefanyika Jumapili hii, chama cha mrengo wa kushoto cha Social Democrats (SPD), mshirika mdogo katika serikali, kingepata asilimia 15% ya kura, ambayo ni ongezeko la asilimia 1 na kile cha kijani kusalia katika asilimia 11.

Katika tafiti za hivi majuzi za taasisi nyingine za upigaji kura, AfD ilikuwa kwenye kiwango sawa ama nyuma tu kidogo ya muungano huo wa kihafidhina.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW