Chama cha ANC chafungua kampeni za uchaguzi
24 Februari 2024Chama cha ANC kinaangazia namna ya kukabiliana na ghadhabu iliyochochewa na ukosefu wa ajira, kuzorota kwa uchumi na kuutetea wingi wa wafuasi wake waliodumu kwa miongo mitatu iliyopita.
Akitangaza uzinduzi wa ilani ya uchaguzi mkuu wa Mei 29, kiongozi wa chama hicho rais Cyril Ramaphosa ameahidi kukitumia kipindi cha miezi mitatu iliyosalia kuwaeleza wafuasi wao juu ya umuhimu wa ANCkusalia kama chaguo bora katika uchaguzi wa 2024.
Aidha ameahidi kufanya mchujo wa kina kwa wagombea wa nyadhifa mbalimbali kupitia chama hicho ambao wameonekana kukumbwa na kashfa katika siku za karibuni.
Chini ya uongozi wa Rais Cyril Ramaphosa ANC imeshuhudia kupungua kwa kiasi kikubwa uungwaji mkono kutokana na madai ya ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi na sasa kinakabiliwa na kizingiti kikubwa cha kutetea wingi wa kutosha bungeni katikati ya mashaka ya kupoteza katika jimbo muhimu la Kwazulu-Natal.