1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBangladesh

Chama cha BNP Bangladesh chadai ushindi kwa wingi bungeni

13 Februari 2026

Chama cha Bangladesh Nationalist Party (BNP) kimedai ushindi katika uchaguzi wa kwanza uliofanyika jana, hatua inayokiweka kwenye nafasi ya kuunda serikali ijayo na kurekebisha sura ya siasa za nchi hiyo.

Bangladesh Dhaka 2026 | Jamaat-e-Islami-Kiongozi-Shafiqur Rahman akipiga kura
Chama cha upinzani cha Jamaat-e-Islami kimeeleza wasiwasi wa ucheleweshwaji wa kutangazwa matokeo rasmi ya uchaguzi wa bunge nchini Bangladesh, ambako chama cha Bangladesh Nationalist kimetangaza kushinda Picha: Zabed Hasnain Chowdhury/ZUMA/IMAGO

Kupitia mtandao wa X,  BNP imedai kupata viti vya kutosha kuunda serikali, ingawa chama hasimu, Jamaat-e-Islami, kilieleza wasiwasi kuhusu ucheleweshaji wa kutangaza matokeo rasmi. BNP inaongozwa na Tarique Rahman mwenye umri wa miaka 60, anayewania nafasi ya waziri mkuu, ambaye alirejea Bangladesh mwezi Desemba baada ya kuishi uhamishoni London kwa miaka 17.

Tume ya Uchaguzi bado haijatoa matokeo ya mwisho, lakini vyombo kadhaa vya habari vya ndani vimeripoti kuwa BNP imevuka idadi ya viti 151 vinavyohitajika kupata wingi wa wabunge katika Bunge lenye jumla ya viti 350, ikiwa ni pamoja na viti 50 maalumu kwa wanawake vinavyogawiwa kwa uwiano wa ushindi wa vyama.

Huu ni uchaguzi wa kwanza baada ya mapinduzi ya umma yaliyoongozwa na vijana kumng'oa madarakani Waziri Mkuu Sheikh Hasina mwaka 2024.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW