1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Chama cha Imran Khan chapata mwenyekiti mpya

2 Desemba 2023

Mmoja wa wanasheria wa waziri mkuu aliyeondolewa madarakani nchini Pakistan, Imran Khan, Barrister Gohar Ali Khan amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama cha kiongozi huyo.

Pakistan | Khan-Urteil
Waziri Mkuu wa Zamani wa Pakistan aliye gerezani, Imran KhanPicha: Akhtar Soomro/REUTERS

Hatua ambayo inakipa nafasi chama cha Khan kushiriki katika uchaguzi ambao umepangwa kufanyika Februari mwakani.Mwanasheria Barrister alikuwa ameteuliwakuwa mwenyekiti wa Pakistan Tehreek-e-Insaaf (PTI), na Khan mwenyewe aliye gerezani na kuzuiwa kushiriki uchaguzi.Tume ya Uchaguzi ya Pakistan ilikuwa imeagiza PTI ifanye uchaguzi wa mwenyekiti wake mpya ikiwa kingetaka kushiriki uchaguzi wa mkuu wa  Februari 8.Chama cha PTI kitakabiliana na upinzani mkubwa kutoka katika chama cha waziri mkuu wa zamani Nawaz Sharif. Lakini wakili aliyechaguliwa Jumamosi hii hatolazimika kuwa waziri mkuu, endapo chama chake kitashinda.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW