Chama cha Kabila chasema hukumu dhidi yake ni ya kisiasa
1 Oktoba 2025
Matangazo
Katibu Mkuu wa chama hicho, Emmanuel Ramazani Shadary amesema wanaamini ni wazi kuwa nia ya utawala wa kidikteta uliopo madarakani ni kumtenganisha Kabila na siasa.
Jana, Mahakama ya Kijeshi ilimuhukumu Kabila adhabu hiyo baada ya kukutwa na hatia ya kuliunga mkono kundi la waasi wa M23, ambalo limechukua udhibiti wa eneo la mashariki mwa Kongo.
Hata hivyo, Kabila, alihukumiwa bila ya kuwepo mahakamani.
Richard Bondo, wakili aliyeyawakilisha majimbo ya Kivu Kusini na Kaskazini amesema ameridhishwa na uamuzi wa mahakama.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameonya kuwa hukumu dhii ya Kabila inaweza kuongeza mgawanyiko katika taifa hilo kubwa lenye utajiri wa madini, ambalo limekumbwa na vita na ukosefu wa utulivu kwa zaidi ya miongo mitatu.