1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Olaf Scholz ashinikizwa kutowania tena ukansela

18 Novemba 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz siku ya Jumapili alikabiliwa na shinikizo kubwa kutoka ndani ya chama chake la kutowania kwa mara nyingine ukansela.

Kansela Olaf Scholz akiwa Potsdam 2024
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz anakabiliwa na shinikizo la kuachia ngazi na kumpa nafasi Waziri wa Ulinzi Oscar PistoriusPicha: Fabian Sommer/dpa/picture alliance

Chama hicho badala yake kinamtaka asafishe njia kwa Waziri wa Ulinzi Boris Pistorius kupitia chama hicho cha Social Democrats (SPD) katika uchaguzi mkuu ujao.

Joe Weingarten na Johannes Arlt, ndio wabunge wa kwanza wa SPD kumpigia debe Pistorius ambaye ni maarufu zaidi kuliko Scholz, kulingana na kura za maoni.

Mnamo mwezi Julai, Scholz alitangaza nia yake ya kuwania tena ukansela, miezi kadhaa kabla ya kuporomoka kwa serikali ya mesto wiki iliyopita.

Kufuatia kuporomoka kwa serikali inayoongozwa na Scholz, kura ya Imani imeshapangwa na uchaguzi wa mapema vilevile unatarajiwa kufanyika Februari badala ya Septemba.

Hata hivyo Scholz amesimama kidete na mpango wake akisema yeye na chama cha SPD wako tayari kwa michakato hiyo kw alengo la kushinda.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW