1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha Kijani champitisha Habeck kuwania ukansela

17 Novemba 2024

Chama cha Kijani cha walinzi wa mazingira nchini Ujerumani kimemchagua kwa asilimia 96.48 ya kura Waziri wa Uchumi, Robert Habeck, kuwa mgombea wa ukansela atayekiwakilisha chama hicho katika uchaguzi ujao.

Uchaguzi, Ujerumani, 2025
Waziri wa Mambo wa Nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock (wa pili kulia) akimkumbatia kwa kumpongeza Robert Habeck kwa kuchaguliwa kuwania ukansela kupitia chama chao cha Kijani.Picha: Thomas Lohnes/Getty Images

Hatua hiyo ilifikiwa kwenye kongamano la chama hicho lililomalizika siku ya Jumapili (Novemba 17).

Habeck alikuwa na nafasi kubwa zaidi ya kuchaguliwa kukiongoza chama hicho.

Soma zaidi: Serikali ya Ujerumani yasambaratika kutokana na uchumi unaoyumba

Waziri wa Mambo ya Nje, Annalena Baerbock, aliyegombea ukansela kwa tiketi ya chama hicho kwenye uchaguzi wa mwaka 2021 amempongeza Habeck kwa kuchaguliwa kukiwakilisha chama cha Kijani.  

Habeck, ambaye pia ni makamu wa kansela katika serikali ya Kansela Olaf Scholz, wiki hii alithibitisha mipango yake ya kugombea nafasi hiyo ya juu.