1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha kisoshalisti Moldova chapinga ushindi wa Sandu

4 Novemba 2024

Chama cha kisoshalisti nchini Moldova kinachopendelea mahusiano ya karibu na Urusi leo kimekataa kuyatambua matokeo yaliyompa ushindi Rais Maia Sandu katika uchaguzi wa duru ya pili uliofanyika jana Jumapili.

Rais Maia Sandu wa Moldova
Rais Maia Sandu wa MoldovaPicha: Rodion Proca/SNA/IMAGO

Taarifa iliyotolewa na chama hicho imesema hakimtambui Sandu kuwa rais halali kikisema ushindi wake unatambuliwa pekee na wafadhili wake pamoja na wauungaji wake mkono kutoka nje.

 Chama hicho kimedai ushindi Sandu umepatikana chini ya vitendo vya hujuma dhidi ya wapiga kura na kwamba umma wa taifa hilo unahisi kusalitiwa na kuporwa sauti yao. 

Soma pia:Moldova: Rais Sandu ashinda uchaguzi wa urais uliorudiwa

Sandu, mwanasiasa anayependelea sera zinazoiweka karibu Moldova na mataifa ya Magharibi, alishinda muhula wa pili madarakani kwa kupata asilimia 55 dhidi ya mpinzani wake mkuu anayeegemea upande wa Urusi, Alexandr Stoianoglo, aliyeambulia asilimia 45. 

Uchaguzi huo huo uliofanyika jana ulishuhudia madai ya uingiliaji wa Urusi, udanganyifu na vitisho dhidi ya wapiga kura. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW