1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha Labour Uingereza chaandikisha matokeo mabaya

9 Mei 2026

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer ameahidi kuimarisha serikali yake inayopitia misukosuko, huku akikabiliwa na miito ya kujiuzulu baada ya matokeo mabaya ya chama chake cha Labour kwenye chaguzi za mitaa na kikanda.

Uingereza  London 2026 | Starmer verlässt Downing Street
Waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer akiondoka afisini mwake mjini London mnamo Aprili 20, 2026Picha: Justin Ng/Avalon/IMAGO

Matokeo ya mwisho yaliowasilishwa leo Jumamosi, yameonyesha kuwa chama cha Labour kimepoteza viti 1,000 vya udiwani kote Uingereza na kuondolewa mamlakani huko Wales baada ya kuongoza kwa miaka 27.

Chama kinachopinga uhamiaji cha Reform UK kimeshinda karibu viti 1,300 kote nchini Uingereza, huku kikishika nafasi ya pili huko Wales na kupata mafanikio makubwa nchini Scotland.

Matokeo hayo yanaonekana na wengi kama kura ya maoni isiyo rasmi dhidi ya  Starmer,  ambaye umaarufu wake umeshuka tangu alipochukuwa uongozi wa chama hicho cha Labour takriban miaka miwili iliyopita.

Hata hivyo hii leo, Starmer amesisitiza kuwa hataondoka na kuitumbukiza nchi hiyo katika mparaganyiko, na kusema kwamba matokeo hayo hayajaleta changamoto ya moja kwa  moja kwa uongozi wake.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW