1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha siasa kali Uholanzi chajipanga kuunda serikali

23 Novemba 2023

Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia nchini Uholanzi, ambacho kinaupinga Umoja wa Ulaya, cha Freedom Party kinatarajiwa kuunda serikali mpya ya nchi hiyo baada ya kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa bunge.

Niederlande Amsterdam | Parlamentswahl
Wapiga kura wa Uholanzi wakishiriki haki yao ya msingi ya kupiga kura katika uchaguzi wa bungePicha: Piroschka van de Wouw/REUTERS

Kiongozi wa chama hicho, Geert Wilders leo ataanza mchakato wa kutafuta washirika wa kuunda nae serikali ya mseto. Wilders ambaye ni shabiki mkubwa wa rais wa Hungary anayeupinga Umoja wa Ulaya, Viktor Orban na ambaye anawachukia Waislamu ameahidi kusitisha mipango yote ya kupokea wahamiaji, kukata malipo yanayotolewa na Uholanzi kwa Umoja wa Ulaya, pamoja na kuzuia hatua ya kukaribisha mwanachama yoyote mpya katika Umoja huo ikiwemo Ukraine.

Somza pia:Waholanzi wapiga kura kumchagua waziri mkuu mpya

Frans Timmermans,ni mwanasiasa kutoka muungano ulioshindwa wa vyama vya Groen Links na labour ,ameezungumzia juu ya kuvunjwa moyo na matokeo ya uchaguzi kwa kusema. Tutawaonesha kwamba kupitia mshikamano,inawezekana kuwa na Uholanzi tofauti na bora.Kwa pamoja tutawashawishi wale watu ambao bado hawajaelewa ni kitu gani kiko hatarini,lakini ambao wataelewa hicho katika siku na wiki zijazo.Kwa pamoja na wao tukiwa na mshikamano tutaifanya Uholanzi kuwa bora.Naanimini katika hillo,na nyinyi mnaamini hivyo? Waislamu nchini Uholanzi wanawasiwasi kuhusu mustakabali wao kufuatia ushindi wa chama cha siasa kali cha Freedom Party.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW