1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha Social Democratic chazindua kampeni ya uchaguzi

5 Desemba 2024

Chama cha Social Democratic kimezindua kampeni zake za uchaguzi na kuahidi kuubadilisha mkondo wa vipaumbele vyake. Scholz ameonesha mtazamo wa kujiamini katika ujumbe wake alipowahutubia wanachama wa chama chake wa SPD.

Scholz | Kansela | Ujerumani
Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Kansela Scholz amekiambia chama chake cha Social Democratic, SPD kwamba uchaguzi mkuu utakaofanyika mnamo mwezi Februari mwakani ni muhimu kwa sababu ndio utakaoamua juu ya mustakabali wa Ujerumani.

Scholz alitamka hayo mbele ya wanachama wa chama chake wapatao 500 mjini Berlin.

"Bunge jipya la Ujerumani litachaguliwa tarehe 23 Februari mwakani. Hatuna muda wa kupoteza. Tunapaswa kujitokeza kote nchini sasa. Mambo mengi yamo hatarini.Tunapaswa kufanya maamuzi ya kimsingi kwa nchi yetu kwa kila namna. Ikiwa tutafanya makosa, basi yataleta madhara makubwa."

Kansela Olaf Scholz amesema, mnamo siku zijazo, kabla ya uchaguzi atafanya kila linalowezekana kwa manufaa ya nchi na ya chama chake cha SPD.

Scholz: Tunaweza kubadilisha hali ya mambo

Chama cha waliberali, FDP kinachoongozwa na aliyekuwa waziri wa fedha Christian Lindner akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho. Picha: Christoph Soeder/dpa/picture alliance

Licha ya chama chake kuanguka katika kura za maoni, Scholz na kiongozi wa chama hicho Lars Klingbeil wameahidi kuwa chama hicho kitaweza kuibadilisha hali.

Hususan Klingbeil ameonesha matumaini makubwa juu ya chama chake na amesema wanachama wake wana motisha mkubwa juu ya kampeni za uchaguzi. Amesema wanachama wake wamesimama pamoja kwa uthabiti.

Taarifa iliyofichuka juu ya mpango wa chama cha waliberali juu ya kuihujumu serikali ya mseto ya Kansela Scholz, imempa mtaji wa kisiasa Kansela wa Ujerumani na mambo kwa hakika yameanza kubadilika.

Soma pia: Robert Habeck kuchaguliwa kukiongoza chama cha Kijani

Chama cha waliberali, FDP kinachoongozwa na aliyekuwa waziri wa fedha Christian Lindner, kilikuwamo katika serikali hiyo ya mseto kabla ya kujiondoa na  kusababisha serikali hiyo ivunjuke. Kansema Scholz ameeleza.

Katika hotuba yake Kansela Scholz alimkosoa vikali, aliyekuwa waziri wake wa fedha Lindner, kwa kula nja za kuihujumu serikali yake.

"Bwana Lindner na chama chake cha FDP, kwa mtindo mmoja walizihujumu kazi za serikali kuu kwa miezi kadhaa. Walitaka sana kuyazuia mafanikio ya serikali, hawakutaka tufanikiwe. Ndugu zangu, jambo kama hili halipaswi kutokea tena nchini Ujerumani."

Kansela wa Ujerumani afanya ziara ya kwanza barani Afrika

01:24

This browser does not support the video element.

Kansela huyo ameeleza kuwa uchaguzi nchini Ujerumani huamuliwa kutokana na sera za mrengo wa kati. Ameeleza kwamba hiyo imekuwa hivyo wakati wote na itaendelea kuwa hivyo, pia katika uchaguzi ujao wa mwezi Februari.

Amesema chama chake cha SPD ndiyo nguzo ya demokrasia nchini Ujerumani. Sio CDU cha Friedrich Merz, wala chama cha kijani.

Soma pia: Scholz, Putin wazungumza kwa mara ya kwanza tangu 2022 

Utafiti mmoja wa maoni, unaonesha kwamba Kansela Scholz anaimarika katika kuungwa mkono na wapiga kura dhidi ya mpinzani wake mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani, cha CDU Friedrich Merz, ambaye ni mgombea wa ukansela kwa niaba ya chama hicho.

Takwimu zinaonesha ongezeko la asilimia 7 kwa chama cha SPD katika wiki iliyopita. Hata hivyo, asilimia 30 ya wapiga kura wanasema watampigia kura, kiongozi wa upinzani Friedrich Merz.

Wakati huo huo, asilimia 16 wamesema wangemchagua Robert Habeck, wa chama cha Kijani ambaye ameshuka kidogo katika kura za maoni ikilinganishwa na wiki iliyotangulia.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW