SPD Berlin chagawika kuhusu kuungana na wahafidhina
6 Machi 2023Hatua ya Giffey ya kupendelea kuunda serikali na chama cha CDU imepingwa na kambi ya chama chake mwenyewe, SPD. Hivi karibuni vyama hivyo viwili vitangaza vitaingia kwenye mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto baada ya CDU kupata ushindi usiokuwa wa kawaida katika uchaguzi wa jimbo hilo mwezi uliopita na chama cha Kansela Olaf Scholz SPD kikaibuka nafasi ya pili.
Giffey kwa sasa anaongoza muungano na vyama vya Kijani na kile cha mrengo mkali wa kushoto cha Die Linke. Hata hivyo uamuzi huo umekigawa chama. Mji wa Berlin ni moja kati ya majimbo 16 yanayounda shirikisho la Ujerumani.
Jumuiya ya wilaya ya Giffey, katika kitongoji cha Berlin kusini ya Neukölln, ilipitisha kwa wingi mdogo hoja ya tawi la vijana la SPD la Jusos siku ya Jumamosi kukataa muungano na CDU, naibu kiongozi wa kundi la chama hicho katika bunge la wilaya Marco Preuß, aliandika kwenye Twitter.