1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha SPD chaongoza kwa ushindi mwembamba Brandenburg

22 Septemba 2024

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa jimbo la Brandenburg yakipa ushindi mwembemba chama cha Kansela Olaf Scholz cha SPD.

Dietmar Woidke, Kiongozi wa SPD Brandenburg
Dietmar Woidke, Kiongozi wa SPD BrandenburgPicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Chama cha Kansela Olaf Scholz cha Social Democratic SPD kimepata ushindi mwembamba katika uchaguzi wa jimbo la Brandenburg. SPD kiko mbele ya chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha AfD  kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotangazwa jioni hii Jumapili, 22.09.2024.

Chama cha SPD kikiongozwa na mgombea wake katika jimbo hilo Dietmar Woidke kimepata asilimia 32 ya kura huku AfD kikijikingia asilimia 29 kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotangazwa na kituo cha umma cha ZDF.

Viongozi wa AfD Hans-Christoph Berndt na Björn Höcke, Picha: Christoph Soeder/dpa/picture alliance

Matokeo yaliyotangazwa na kituo kingine cha utangazaji cha ARD kimesema SPD kinaongoza kwa asimilia 31 huku AfD kikiwa na asilimia 30. Matokeo yanaonesha pia vyama vya Kijani na Die Linke viko chini ya asilimia tano.

Wapiga kura katika jimbo la mashariki mwa Ujerumani la Brandenburg walipiga kura katika uchaguzi uliofuatiliwa kwa karibu,huku nchi ikiwa katika shauku  kuona je mara hii chama cha siasa kali za mrengo wa kulia kitaungwa mkono kwa kiwango kikubwa,kama ilivyokuwa katika uchaguzi wa jimbo la  Thuringia ,au ikiwa chama cha Social Democratic,SPD kitaibuka mshindi.

SPD ni chama kinachoongozwa na Kansela Olaf Scholz lakini pia kimekuwa kikiungwa mkono katika jimbo hilo la Brandenburg kikiongozwa na Dietmar Woidke.Soma pia: Serikali ya muungano ya Ujerumani kuyumbishwa na matokeo ya majimbo

Furaha yatawala ofisi za SPD BrandenburgPicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Brandenburg, ni jimbo pekee la iliyokuwa Ujerumani Mashariki ambalo limeendelea kutawaliwa tangu 1990 na chama cha SPD ambacho kimekuwa kikishirikiana katika serikali ya mseto  na vyama vingine.Woidke mwenye umri wa miaka 62 ameliongoza jimbo la Brandenburg kwa miaka 11 iliyopita.

Kura za maoni zilizochapishwa alhamisi na kituo cha habari cha Ujerumani cha ZDF zilionesha chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha AfD kitashinda kwa asilimia 28 ya kura kwenye jimbo hilo huku SPD ikipata asilimia 27 na chama cha wahadhina cha CDU kikipata asilimia 14 huku chama kipya cha muungano wa Sahra Wagenknecht  (BSW) kikipata asilimia 13.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW