Chama cha SPD chashindwa Rhineland-Palatinate
23 Machi 2026
Katika uchaguzi mwingine wa majimbo nchini Ujerumani uliofanyika jana Jumapili kwenye jimbo la Rhineland-Palatinate, chama cha Social Democratic SPD kilishindwa kwa mara nyingine.
Baada ya kuliongoza jimbo hilo la Kusini Magharibi mwa Ujerumani kwa kiasi miaka 35 chama hicho kimebanduliwa uongozini na chama cha Kansela Friedrich Merz cha CDU.
Matokeo ya awali yanaonesha kwamba chama cha CDU kimeibuka mshindi kwa kupata asilimia 31, kikifuatiwa na SPD kilichojinyakulia asilimia 25.9 ya kura.
Chama cha Christian Democratic Union chapata pigo chaguzi za majimbo
Matokeo hayo ndiyo mabaya zaidi kwa Wasoshalisti katika jimbo hilo ambacho katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2021 kilipata asilimia 35.7.
Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha AfD kilijiongezea umaarufu kikishikilia nafasi ya tatu kwa kupata asilimia 19.5 ambayo ni matokeo yao mazuri ya kihistoria Magharibi mwa Ujerumani.