1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha UDPS cha ongoza matokeo ya uchaguzi wa bunge Kongo

Saleh Mwanamilongo
14 Januari 2024

Chama tawala nchini Kongo UDPS kimepata viti 66 vya bunge miongoni mwa 500 kwenye bunge la nchi hiyo, lakini miungano ya vyama vinavyomuunga mkono Tshisekedi vimezowa viti kadhaa.

Matokeo ya uchaguzi yameonyesha chama tawala cha UDPS kikiongoza kwa kupata viti 66 bungeni
Matokeo ya uchaguzi yameonyesha chama tawala cha UDPS kikiongoza kwa kupata viti 66 bungeniPicha: ARSENE MPIANA/AFP

Chama cha UDPS cha Rais wa Kongo Felix Tshisekedi kimeshinda asilimia 12 ya viti vya bunge katika uchaguzi wa Desemba, na kukiweka mbele ya vyama 44 vingine vilivyoshinda kiti kimoja au zaidi katika viti 500 kwenye bunge la nchi hiyo.

Kwenye matokeo ya uchaguzi yaliotangazwa na Tume ya Uchaguzi nchini Kongo, CENI, chama cha UDPS kimepata viti 66, kutoka viti 35 vya ubunge kwenye uchaguzi wa mwaka wa 2018.

Kwa mujibu wa matokeo hayo, hata hivyo rais Tshisekedi pamoja na vyama washirika watakuwa na wingi wa viti bungeni. Matokeo ya muda yaliyotangazwa na Tume ya uchaguzi yameonyesha kuwa vyama vinavyoongozwa na baadhi ya Washirika wa Tshisekedi akiwemo Spika wa Seneti Modeste Bahati Lukwebo, Waziri wa Ulinzi Jean Pierre Bemba na Waziri wa Uchumi Vital Kamerhe vilishinda kwa jumlya zaidi ya viti Themanini vya bunge. Upinzani umelalamikia kasoro za uchaguzi huo na kutaka urudiwe.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW