1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani wapata kura nyingi, Lagos Nigeria

Hawa Bihoga
27 Februari 2023

Mgombea wa chama cha Labour Peter Obi amemshinda mpinzani wake wa chama tawala mjini Lagos katika matokeo yaliotangazwa hivi punde, baada ya uchaguzi uliokumbwa na ucheleweshwaji na malalamiko ya ukiukwaji wa taratibu.

Nigeria | Wahltag
Picha: Uwais Abubakar Idris/DW

Kulingana na tume huru ya uchaguzi nchini humo Obi amepata kura 582,454 , wakati gavana wa zamani wa Lagos na mgombea wa chama tawala, Bola Tinubu, akipata kura 572,606.

Mgombea wa chama kikuu cha upinzani cha People's Democratic Party, Atiku Abubakar ameshika nafasi ya tatu kwa kupata kura 75,750.

Mgombea upinzani ashinda urais jimbo la Lagos

Tathmini ya awali inaonesha Tinubu anaongoza katika maeneo mengi, ingawa theluthi mbili ya majimbo katika taifa hilo lenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika yalikuwa bado hayajatangaza matokeo yake.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW