1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMsumbiji

Upinzani nchini Msumbiji waomba kura kuhesabiwa upya

28 Oktoba 2024

Chama kikuu cha upinzani nchini Msumbiji cha Podemos kimefunguwa kesi mahakamani kudai kura za uchaguzi mkuu uliopita zihesabiwe upya.

'Obtimist Party for the Development of Mozambique' (PODEMOS) chataka kura kuhesabiwa upya
Aliyegombea urais kupitia chama cha 'Obtimist Party for the Development of Mozambique' (PODEMOS) Venancio Mondlane, akizungumza na waandishi wa habari.Picha: Alfredo Zungia/AFP

PODEMOS imechukuwa uamuzi huo baada ya kuongoza maandamano makubwa na vurugu kutokana na chama tawala cha Frelimo kutangazwa mshindi kwenye uchaguzi wa rais na bunge wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa nyaraka zilizoonekana na shirika la habari la AFP, kesi iliyofunguliwa na chama cha upinzani cha PODEMOS, jana Jumapili inataka Mahakama ya Katiba kutowa uamuzi wa juu ya mshindi wa kweli wa uchaguzi huo.

Chama hicho kinaitaka mahakama itowe uamuzi wa kuhesabiwa tena kura zote, kikisema uchaguzi wa tarehe 9 ulikumbwa na dosari.

Chama hicho pia kimesema kimewasilisha ushahidi mbele ya tume ya uchaguzi,- wa maboksi kadhaa ya nyaraka zinazoonesha kilishinda uchaguzi.