1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSlovakia

Chama kinachopendelea usuhuba na Urusi chashinda Slovakia

1 Oktoba 2023

Chama cha mrengo wa kushoto kinachopendelea mahusiano ya karibu na Urusi kimeshinda uchaguzi wa Bunge nchini Slovakia.

Waziri Mkuu wa zamani wa Slovakia na kiongozi wa muungano wa SMER-SSD,  Robert Fico
Waziri Mkuu wa zamani wa Slovakia na kiongozi wa muungano wa SMER-SSD, Robert FicoPicha: Radovan Stoklasa/REUTERS

Matokeo hayo yanayoashiria uwezekano wa mageuzi makubwa ya sera ya kigeni kwenye taifa hilo dogo la Ulaya itaijongelea Moscow.

Matokeo ya mwisho yanaonesha chama hicho cha Smer-SSD chenye misimamo ya kupinga msaada wa kijeshi kwa Ukraine na kuzikosoa sera za Umoja wa Ulaya kimepata asilimia 23.3 ya kura na kukizidi chama cha siasa za wastani cha Progressive Slovakia kilichokuwa madarakani.

Ushindi huo unaamaanisha chama hicho kinachoongozwa na waziri mkuu wa zamani Robert Fico kimepata idadi ya viti 42 kati 150 vya Bunge la Slovakia na kitahitaji washirika wadogo ili kuunda serikali.

Wakati wa kampeni, Fico aliahidi serikali yake haitopeleka "risasi hata moja" nchini Ukraine, msimamo ambao wafuatiliaji wa siasa za Ulaya wanasema unafanana na waziri mkuu wa Hungary, Victor Orban.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW