SiasaJapan
Chama tawala nchini Japan chamteua mwanamke kuwa Mwenyekiti
6 Oktoba 2025
Matangazo
Sanae Takaichi mwenye umri wa miaka 64, ni mhafidhina mwenye msimamo mkali ambaye anatarajiwa kuwa waziri mkuu wa kwanza mwanamke nchini humo, atahitaji kutafuta njia za kukidumisha madarakani chama chake cha Kiliberali na kupata tena uungwaji mkono wa umma kwa kuchukua hatua za kushughulikia tatizo la mfumuko wa bei na kukabiliana na changamoto mbalimbali za kidiplomasia.
Bi Sanae Takaichi ambaye ni mfuasi mkubwa wa maono ya kihafidhina ya Waziri Mkuu wa zamani wa Japan Shinzo Abe, yuko kwenye hatihati ya kupoteza ushirika wa muda mrefu wa chama cha siasa za mrengo wa kati cha Komeito kutokana na siasa zake za kihafidhina.