1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJamhuri ya Moldova

Chama tawala cha Moldova chaongoza uchaguzi wa bunge

29 Septemba 2025

Chama tawala cha Moldova na kinachounga mkono Umoja wa Ulaya kinaongoza kwenye uchaguzi wa bunge hii ikiwa ni kulingana na kura ambazo tayari zimehesabiwa hadi mapema siku ya Jumatatu.

Moldova Chisinau 2025 | Kituo cha kupigia kura katika uchaguzi wa bunge la Moldova uliokumbwa na madai ya uingiliaji wa Urusi
Kituo cha kupigia kura katika uchaguzi wa bunge la Moldova uliokumbwa na madai ya uingiliaji wa Urusi, Septemba 28, 2025Picha: Paul Dza/SIPA/picture alliance

Uchaguzi wa Jumapili ulionekana kuwa muhimu kwa nchi hiyo katika kuendeleza msukumo wake wa kujiunga na Umoja wa Ulaya. Msukumo huo ulianza baada ya Urusi kuivamia Ukraine, mwaka 2022.

Huku asilimia 95 ya kura zikiwa zimekwishahesabiwa hadi mapema leo, Chama cha Action and Solidarity (PAS), kilicho madarakani tangu 2021, kilikuwa kinaongoza kwa asilimia 48.3, huku Kambi inayounga mkono Urusi ya Patriotic ikiwa na asilimia 25.5.

Taifa hilo dogo linalowania kujiunga na Umoja wa Ulaya linalopakana na Ukraine na ambalo lina eneo linaloiunga mkono Urusi, limegawanyika kwa muda mrefu kuhusu ama kujiunga na umoja huo au kuendeleza uhusiano na Moscow ulioanzia enzi ya Sovieti.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW