1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama tawala cha zamani NCP chapigwa marufuku Sudan

Oumilkheir Hamidou
29 Novemba 2019

Viongozi wepya wa Sudan wameamuru chama cha rais aliyeng'olewa madarakani Omar al Bashir kivunjwe na " kukongolewa" mabaki ya utawala wake wa karibu miaka 30.

Sudans neuer Premierminister Abdalla Hamdok
Picha: picture-alliance/AP Photo

Kwa kufanya hivyo  viongozi hao wapya wameitika wito wa waandamanaji  ambao kilio chao kilipelekea kupinduliwa al Bashir. 

Omar al Bashir na chama chake cha itikadi kali cha National Congress-NCP wameitawala nchi hiyo ya kaskazini mashariki mwa Afrika tangu mwaka 1989 kabla ya wimbi kubwa la maandamano kupiga kote nchini na kuwang'owa madarakani mapema mwaka huu.

Halmashauri  huru ya uongozi wa taifa na baraza la mawaziri linaloongozwa na waziri mkuu Abdallah Hamdok wamepitisha uamuzi wa kukivunja chama hicho na kupitisha sheria ya "kukongowa utawala wa juni 30 mwaka 1989."

"Chama cha National Congress kimevunjwa na kimefutwa katika madaftari ya vyama vya kisiasa vilivyosajiliwa nchini Sudan" sheria hiyo inasema na kuongeza kamati maalum itaundwa ili kuwapokonya milki yote waliyonao.

"Hakuna  yeyote anaejitambulisha na chama hicho atakaeruhusiwa kujishughulisha  na siasa kwa kipindi cha miaka kumi inayokuja."Umauzi wa kukivunja chama sio kisasi dhidi ya watawala wa zamani-amesema Hamdok kupitia mtandao wa twitter."Umelenga  kulinda hadhi na murwa wa wananchi wa Sudan . Sheria hiyo imelengwa kurejesha mali ya wananchi iliyoporwa.

Vuguvugu la wapenda mageuzi ya kidemokrasiPicha: Reuters/M. N. Abdallah

Wanaharakati wanaopigania mageuzi wanasifu sheria hiyo

Wajdi Salah msemaji wa vuguvugu la waandamanaji wanaopigania Uhuru na Mageuzi amesema katika ukurasa wake wa Facebook kwamba "chama tawala cha zamani kitavunjwa moja kwa moja."

Jumuia ya wasomi wa Sudan, kundi la wanaharakati walioanzisha maandamano dhidi ya al Bashir wameusifu uamuzi huo."Ni hatua muhimu katika kulifikia lengo la mapinduzi na kufungua njia ya kuunda taifa linaloheshimu demokrasia ya raia.-imesema jumuia hiyo katika taarifa yake.

Halmashauri huru ya uongozi wa taifa na baraza la mawaziri wamebatilisha pia sheria inayobishwa iliyokuwa ikibana haki za wanawake chini ya utawala wa Omar al Bashir. Maelfu ya wanawake waliteswa, walitozwa faini au hata kufungwa chini ya sheria hiyo ambayo wanaharakati wanasema iliwalenga wanawake kwa misingi ya sheria kali za dini ya kiislam.

Rais wa zamani wa Sudan Omar el BashirPicha: Getty Images/AFP/E. Hamid

NCP kinasema hakitishiki

Chama cha rais aliyepinduliwa , NCP kimelaani uamuzi wa viongozi wepya wa Sudan wa kukipiga marufuku  na kusema hawatshiki na amri yoyote au sheria kwakuwa wanatambua wao wana nguvu na fikra zao  zitadumu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW