1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama tawala Georgia chashinda uchaguzi wa bunge

Sylvia Mwehozi
27 Oktoba 2024

Chama tawala nchini Georgia kimeshinda uchaguzi wa bunge kulingana na tume ya uchaguzi, baada ya upinzani kulalamikia matokeo,ukisema ni ya udanganyifu.

Wafuasi wa Chama tawala nchini Georgia wakifurahia matokeo
Wafuasi wa Chama tawala nchini Georgia wakifurahia matokeoPicha: Irakli Gedenidze/REUTERS

Chama tawala nchini Georgia kimeshinda uchaguzi wa bunge kulingana na tume ya uchaguzi, baada ya upinzani kulalamikia matokeo,ukisema ni ya udanganyifu. Umoja wa Ulaya ulionya kwamba kura hiyo ya Jumamosi ambayo ilikuwa kama mtihani kwa demokrasia kwa taifa hilo, ingeamua juu ya nafasi yake kujiunga na muungano wa Ulaya. 

Matokeo rasmi yanaonyesha kuwa chama tawala cha Georgian Dream party kimeshinda kwa 54% ya kura wakati muungano wa vyama vinne vya upinzani vinavyopigia upatu Umoja wa Ulaya, ukiibuka na asilimia 37.58%.

Matokeo hayo yanakipatia chama tawala viti 91 vya kutosha kutawala katika bunge lenye wabunge 150 lakini vikiwa ni pungufu ya viti 113 ya wingi wa kikatiba, iliokuwa ikitafuta kuvipiga marufuku vyama vyote vikuu vya upinzani. Upinzani umesema hautambui matokeo ya uchaguzi na kuyataja kuwa ya udanganyifu.