NPP yakubali kushindwa katika uchaguzi wa rais Ghana
8 Desemba 2024Bawumia amemmpigia simu mpinzani wake John Dramani Mahama wa chama cha upinzani cha National Democratic Congress (NDC) kumpongeza kwa ushindi.
Amesema licha kwamba bado matokeo rasmi ya uchaguzi hayajatangazwa, matokeo ya awali yanaonesha kuwa Mahama, ambaye ni rais wa zamani anaelekea kupata ushindi mkubwa.
Mahama aongoza katika matokeo ya mwanzo ya kura, Ghana
Kulingana na Bawumia, watu wamepiga kura wakitaka mabadiliko, na chama cha NPP kinaheshimu hilo.
Awali NDC ilitangaza kuwa Mahama alikuwa mbele na asilimia 56 ya kura na hiyo inamaanisha chama hicho kimejizolea viti takriban 185 ya kura kati ya 276 vinavyoshindaniwa.
Mahama aliwahi kuwa rais wa Ghana kuanzia mwaka 2012 hadi mwanzoni mwa mwaka 2017.
Ameahidi kulifufua upya taifa hilo kwa kutoa msaada kwa wafanyabiashara vijana na wakulima katika kampeni yake iliyojikita kwa vijana.