1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGhana

Chama tawala Ghana chamteua mgombea wake wa uchaguzi wa 2024

5 Novemba 2023

Chama tawala cha Ghana cha New Patriotic Party (NPP) kimemteua Naibu rais Mahamudu Bawumia kama mgombea wake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2024.

Chama tawala cha Ghana cha New Patriotic Party (NPP) kimemteua Naibu rais Mahamudu Bawumia kama mgombea wake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2024
Chama tawala cha Ghana cha New Patriotic Party (NPP) kimemteua Naibu rais Mahamudu Bawumia kama mgombea wake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2024Picha: picture alliance

Bawumia aliye na miaka 60, mwanauchumi na aliyefanya kazi pia katika benki kuu ya taifa, amehudumu kama naibu rais na amekuwa pia mtu muhimu katika mabadiliko ya sera za kiuchumi katika uongozi wa rais Nana Akufo-Addo, anayetarajiwa kumaliza muda wake January mwaka 2025 baada ya kuitumikia taifa hilo kwa miaka 8 kulingana na katiba ya taifa hilo.

Katika hotuba yake ya kukubali kuwa mgombea wa urais wa chama tawala, Bawumia aliahidi kuijenga upya nchi hiyo iliyoyumba kiuchumi iwapo atachaguliwa kuwa rais wa Ghana.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW