1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama tawala Malawi chalalamikia wizi wa kura

24 Septemba 2025

Chama tawala Malawi cha Rais Lazarus Chakwera cha Malawi Congress, MCP, kimedai kina ushahidi wa wizi wa kura, wakati ambapo matokeo ya awali yanaashiria kuwa kinashindwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika wiki iliyopita.

Malawi Lilongwe 2025 |Uchaguzi wa rais na wabunge
Mwananchi wa Malawi akipiga kuraPicha: Amos Gumulira/AFP

Akizungumza na waandishi habari, Vitumbiko Mumba, mgombea mwenza wa Rais Chakwera, amesema wana ushahidi kuwa baadhi ya watu walikuwa wanajaza karatasi bandia za kupigia kura kwenye masanduku ya kura.

Kwa mujibu wa Mumba, mwanasiasa wa chama cha MCP matokeo ya awali hayalingani na takwimu zilizotangazwa katika kituo cha kuhesabia na kujumlisha kura.

Hata hivyo, chama hicho hakijaonyesha ushahidi wowote ule wa tuhuma hizo.

Mumba amesema chama cha MCP, kimewasilisha malalamiko yake katika Tume ya Uchaguzi ya Malawi, MEC.

Tume hiyo ina muda wa hadi Septemba 24, kutangaza matokeo rasmi ya urais.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW