1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama tawala nchini Malawi chadai kuvurugwa kwa matokeo

20 Septemba 2025

Chama tawala nchini Malawi, Malawi Congress Party (MCP) kimedai kuwepo kwa dosari katika zoezi la kuhesabu kura katika takriban nusu ya wilaya za nchi hiyo baada ya uchaguzi wa wiki hii.

Malawi Lilongwe 2025 |uchaguzi wa urais na bunge
Zoezi la kupiga kura nchini MalawiPicha: Amos Gumulira/AFP

Tume ya Uchaguzi ya Malawi (MEC) ilitoa matokeo yake ya kwanza jana, huku matokeo kutoka kwa mabaraza matatu ya miji kati ya manne yakionyesha ushindi mkubwa kwa Peter Mutharika, mgombea wa upinzani, mwenye umri wa miaka 85.

Lakini muda mfupi kabla ya matokeo hayo, MCP ilisema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba wawakilishi wake wamegundua kasoro za uchaguzi katika wilaya 13 kati ya 28 za nchi hiyo.

Mgombea mwenza wa Rais Lazarus Chakwera wa chama hicho cha MCP Vitumbiko Mumba, amesema MCP imewasilisha malalamiko rasmi kwa tume ya uchaguzi kuhesabu upya kura hasa katika maeneo waliyogundua kasoro kubwa.

Wakati huo huo, polisi nchini humo imesema imewakamata makarani wanane wa data kwa madai ya kuvuruga matokeo hayo ya uchaguzi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW