1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSenegal

Senegal:Pastef yadai kupata ushindi katika uchaguzi wa Bunge

18 Novemba 2024

Chama tawala nchini Senegal kimetangaza kupata ushindi katika uchaguzi wa bunge uliofanyika Jumapili.

Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye wa Chama cha Pastef
Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye wa Chama cha PastefPicha: Zohra Bensemra/REUTERS

Chama cha Pastef chake Rais Bassirou Diomaye Faye, kilikuwa kikisaka wingi wa kutosha bungeni, ili kumuwezesha Faye kutekeleza mageuzi makubwa ya kiuchumi aliyoyaahidi, ikiwa ni miezi minane tangu alipoingia madarakani.

Wapigakura zaidi ya milioni saba waliwachagua wabunge 165 watakaohudumu kwa kipindi cha miaka mitano.  Bunge lilikuwa likiongozwa na upinzani na lilitatiza shughuli za serikali,  jambo ambalo lilimfanya Faye kulivunja bunge mwezi Septemba na kuitisha  uchaguzi wa mapema  mara tu katiba ilipomruhusu kufanya hivyo.

Akiwa nje ya nchi, rais wa zamani Macky Sall anaongoza kundi la upinzani liitwalo Takku Wallu Senegal. Hapo jana, alidai kuwa uchaguzi huo uligubikwa na kile alichokiita "udanganyifu mkubwa ulioandaliwa na chama cha Pastef", bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.

     

    

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW