SiasaUrusi
Chama tawala Urusi chakumbwa na shambulio la mtandaoni
16 Machi 2024Matangazo
Chama hicho tawala kimesitisha utoaji wa huduma zisizokuwa za msingi ili kudhibiti shambulio hilo.
Rais Vladimir Putin ambaye anatetea kiti chake kama mgombea huru japo anaungwa mkono na chama tawala cha United Russia, ameishtumu Ukraine kwa kujaribu kuhujumu uchaguzi huo ambao anatarajiwa kushinda.
Soma pia: Ni yapi malengo ya Rais Putin kwa kuandaa uchaguzi nchini Urusi?
Uchaguzi huo wa siku tatu ulioanza jana, pia unafanyika katika maeneo manne ya Ukraine - Donetsk, Luhansk, Zaporizhzhia na Kherson.
Kulingana na tume ya uchaguzi nchini Urusi, takriban watu milioni 112 wamejiandikisha kama wapiga kura.