1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Champions League: Dortmund yaishinda Chelsea 1-0

16 Februari 2023

Miamba ya soka ya Ujerumani Borussia Dortmund imeichapa Chelsea bao 1-0 katika mechi ya kwanza ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa wanaume.

Fußball Bundesliga Saison 2022/2023 | Jude Bellingham, Borussia Dortmund
Picha: Dennis Ewert/RHR-FOTO/picture alliance

Karim Adeymi alifunga bao pekee la mchezo huo baada ya dakika ya 30. Ushindi huo unaiweka Dortmund katika nafasi nzurikabla ya mechi ya marudiano mjini London mnamo Machi 7.

Dortmund sasa wameshinda michezo yao yote 7 ya mashindano katika Bundesliga, Kombe la DFB na Ligi ya Mabingwa mwaka huu wa 2023.

Soma pia:Union wateleza, Bayern wawanyatia

Siku ya Jumanne, mabingwa wa rekodi ya Bundesliga Bayern Munich walishinda 1-0 wakiwa ugenini dhidi ya klabu ya Lionel Messi, Paris St Germain.

Katika mechi nyingine, Benfica imeshinda 2-0 ugenini dhidi ya Club Bruges Jumatano, na AC Milan waliishinda Tottenham Hotspur Jumanne.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW