Champions League: nani atatinga fainali?
1 Mei 2017Nusu fainali ya kombe la Champions league barani Ulaya inafanyika Jumanne na Jumatano ambapo mabingwa watetezi Real Madrid inakabana koo na majirani zao Atletico Madrid. Real ni timu pekee ambayo imeizuwia Atletico Madrid kuongeza ubingwa wa Champions League katika mafanikio yake chini ya Diego Simeone na kwa mwaka wa nne mfululizo kikosi cha "Rojiblancos" kimezuwia njia ya Atletico kupata taji hilo la Ulaya.
Atletico chini ya kocha wake raia wa Argentina Diego Simeone imeweza kuvifungisha virago vigogo vya soka la Ulaya , kama AC Milan, Chelsea, Juventus , Bayern Munich , na mara mbili Barcelona, lakini wameshindwa mara kadhaa na majirani zao Real madrid. Mchezo mwingine wa nusu fainali utafanyika Jumatano kati ya Monaco inayopambana na Juventus Turin.
Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre / afpe / dpae
Mhariri: Iddi Ssessanga