1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Champions League yarudi tena, nani atatinga robo fainali?

4 Machi 2024

Jumanne mechi za Ligi ya Vilabu Bingwa Ulaya Champions League mzunguko wa pili hatua ya mtoano ya 16 bora zitakuwa zinarindima.

Fußball | UEFA Champions League | Lazio Rom vs Bayern München
Wachezaji wa Bayern Munich wakipambana katika mechi dhidi ya LazioPicha: Alberto Pizzoli/AFP/Getty Images

Real Madrid, Manchester City na Paris Saint Germain wote walipata ushindi kwenye mechi zao za kwanza na wako kifua mbele wanapoingia katika mechi za mzunguko wa pili na wote hawajafungwa katika ligi zao za nyumbani mwaka huu 2024.

Miamba wa Ujerumani Bayern Munich lakini tayari wamepoteza mechi 3 za Bundesliga tangu Januari na katika mechi tano zilizopita kwenye mashindano yote, wampoteza tatu mojawapo ikiwa hiyo ya awamu ya kwanza ya raundi ya 16 bora dhidi ya Lazio nchini Italia walipozabwa 1-0.

Katika miaka 4 iliyopita, Bayern wamefanikiwa kufuzu robo fainali ila msimu huu mambo yanaonekana kuwa tofauti kidogo.

Vyanzo: DPA/AP/Reuters

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW