1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Changamoto kati ya FATAH na HAMAS

13 Juni 2007

Changamoto kati ya wapalestina wenyewe kwa wenyewe inatishia kuongoza katika vita vya kienyeji na mwito unatolewa kwa dola yenye nguvu pengine Misri kuingilia kuhifadhi amani huko Gaza.

Safu za wahariri wa magazeti ya ujerumani hii leo zimetuwama juu ya mada moja tu-machafuko katika mwambao wa gaza kati ya wapalestina wenyewe kwa wenyewe-baina ya chama cha FATAH na chama cha Hamas.Hali ikionekana kama ni vita vya kienyeji vimeripuka,wahariri wajiuliza Mashariki ya kati inaelekea wapi ?

Gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG halioneshi katika uchambuzi wake matumaini mema.Laandika:

“Juhudi za haraka na zenye nguvu zinahitajika kutuliza hali ya mambo.Misri inajaribu.Kwakweli, pangehitajika juhudi za kusaka ufumbuzi kamili wa mzozo wa Mashariki ya kati.Lakini, Israel wakati huu inajisghulisha kufumbua matatizo yake yenyewe na serikali yake ni dhaifu.

Dola kuu Marekani nalo maji yamelifika shingoni tangu nchini Irak hata nchini Afghanistan-kote kuwili kunatokota.Umojawa Ulaya unajitahidi kumpunga shetani kupitia diplomasia.Lakini, haukweza hata kufanikiwa kuwapunguzia hata shida za kimaisha raia wa kipalestina.Kwahivyo, machafuko yatazidi kupambamoto.”

Ni maoni ya Frankfurter Allgemeine Zeitung.

Gazeti la FINANCIAL TIMES la Ujerumani halioni kuna ufumbuzi rahisi wa kitandawili hiki linapochora picha hii:

Katika mwambao wa Gaza mapigano kati ya vyama viwili vya wsapalestina-FATAH na HAMAS ni vigumu kuyatenganisha mbali na vita vya kienyeji.Ugomvi wa vyama hivyo 2 umefikia mpaka ambao dawa iliotumika kutibu hadi sasa si mujarabu tena.Ikiwa iwezekane kumtuliza shetani,basi patahitajika kutumika dawa mpya.

Utulivu kwa hali ilivyo sasa waweza tu kupatikana kwa kujiingiza nguvu ya nje.Vikosi vya kuhifadhi amani kutoka jirani mkubwa Misri,pengine ndio dawa yenye kumzuwia shetani kuzidi kuhemkwa.”

Kwa gazeti la DARMSTÄDTER ECHO mambo ni wazi kabisa ,kwani lamjua nani mkosa hapa:

Wapalestina ambao wsaliounganishwa pamoja na marehemu yasser Arafat aliekosolewa mnona kuwaomngoza katika shabaha ya kuwa na dola lao wenyewe huru,sasa wanaangamiza huko gaza tena makusudi nguzo waliosimamia pamoja katika vita vyao-nayo ni matumaini.Matumaini ya siku moja kuwa na dola lao,matumaini ya amani na usalama.”

Hata gazeti la NEUE OSNABRÜCKER ZEITUNG laandika:

“Hali ya sasa ya machafuko inatokana sana na urithi ulioachwa na Yasser Arafat.Kwa upande mmoja rais huyo wa zamani wa FATAH aliweza kuwaunganisha pamoja wapalestina wote nyuma yake .Kwa upande wapili kupitia na mfumo wa rushua uliostawi chini ya uongozi wake,ndipo chama cha Hamas kilivyowez kujipatia nguvu zake za hii leo.”

Mwishoe, likitufungia ukurasa huu wa safu za wahariri,gazeti la LANDSHUTER ZEITUNG latarajia changamoto kati ya viongozi wa Fatah na Hamas:

“Endapo rais Mahmoud Abbas na waziri wake mkuu Ismail Haniya hawataafikiana haraka kuzima machafuko yanayoendelea kwa muda sasa ,basi vita kamili kati yao havitaweza tena kuepushwa…”