1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Changamoto zinazomkenulia meno Macron

8 Mei 2017

Ushindi wa Emmanuel Macron ni wa kihistoria. Atakuwa rais wa kwanza wa Ufaransa katika miaka ya hivi karibuni asiyetoka katika vyama viwili vikuu. Lakini huenda asipate wabunge wengi kumwezesha katika utawala

Frankreich Hollande und Macron beim Gedenktag in Paris
Picha: picture-alliance/AP Photo/S. de Sakutin

Rais mteule wa Ufaransa Emmanuel Macron ndiye anayefaa kazi hiyo. Anacho kile kinachohitajika kuiongoza Ufaransa, kuiondoa katika mgogoro na kuiweka katika hali thabiti kwenye Umoja wa Ulaya. Lakini hilo halimaanishi kuwa atafanikiwa. Ndivyo anavyosema mwandishi wa DW, Max Hofman.

Huenda isiwe kama ushindi wa Barrack Obama mnamo mwaka 2008. Lakini ushindi wa Emmanuel Macron ni wa kihistoria. Atakuwa rais wa kwanza wa Ufaransa katika miaka ya hivi karibuni asiyetoka katika vyama viwili vikuu vya Wasosholisti na Wahafidhina. Aidha ndiye rais aliyechaguliwa akiwa na umri mdogo.

Kwa wafuasi wake, huu ndio wakati Ufaransa utarejea katika mkondo wake. Kijana, imani na matumaini. Maneno haya yote yanatumiwa na wafuasi wake kuelezea kile wanachokipenda kuhusu rais mpya. Lakini je Macron mwenye umri wa miaka 39 ataweza? Je ataepuka masikitiko makubwa ambayo wengi wameshaona upeoni?

Macron akishangilia ushindi wake mjini ParisPicha: Reuters/P. Wojazer

Macron anayo akili. Akili zaidi! Ndivyo wanavyosema wanaomjua. Katika kila daraja ya maisha yake alitengeneza urafiki na watu werevu nchini Ufaransa: Wafanyabiashara, wanafalsafa, wanasiasa. Mara kwa mara alithibitisha kuwa anaweza kushirikiana, kupatanisha, na kusuluhisha matatizo. Alifanya hivyo akiwa kiongozi wa wanafunzi katika shule bora za Ufaransa na pia kama mjasiriamali katika sekta ya benki.

Kwa wale wanaotilia shaka basi watazame mjadala wa mwisho wa runinga kati yake na mshindani wake Marine Le pen. Macron alikuwa mwepesi, imara na mwelewa wa mambo kuliko mshindani wake. Lakini haya yote yatakuwa bure ikiwa hatapata washirika wakati huu ambapo hali ya siasa za Ufaransa inabadilika.

Siasa ya Macron ni mbichi kama ua changa. Hadi sasa hana hata mwakilishi mmoja katika bunge la Ufaransa. Bila shaka hali hiyo itabadilika ifikapo Juni 18 wakati Wafaransa watawachagua wabunge. Hata hivyo huenda asipate wabunge wengi kumwezesha katika utawala. Anahitaji washirika. Waliopo ni wale ambao walikataliwa na wapigaji kura. Wasoshalisti na wahafidhina.

Waliokataliwa watashirikiana na Macron?

Rais anayeondoka Francois Hollande na rais mteule Emmanuel MacronPicha: Reuters/F. Mori

Vyama vilivyokita mizizi vinafahamu kuwa vitahitajika kushirikiana kwa kiwango fulani. Vikimlemaza Macron kwa manufaa yao wenyewe basi mwishowe vitapoteza. Kwa namna nyingine Wafaransa wanawapa wanasiasa wa zamani nafasi ya mwisho kuwa na wanasiasa wachanga. Walifanya hivyo kwa sababu aliacha serikali ya Hollande miaka miwili iliyopita na kusafisha uvundo uliokuwepo baada ya muda fulani. Ikiwa atashindwa kama watangulizi wake, wapigaji kura wengi huenda wakafikiria kumpigia kura mtu mwengine. Marine Le Pen. Hivyo basi kuna shinikizo tele kwa Macron na watakaokuwa washirika wake bungeni.

Wiki ambazo zimepita zimeonyesha kuwa wasoshalisti wamejipata katika mgogoro kati ya wanaoshikilia siasa za mrengo wa kushoto na kulia. Wahafidhina walimtaka Francois Fillon aliyepoteza kinyang'anyiro alichostahili kushinda. Marine Le Pen ambaye chama chake cha National Front bila shaka kwa mara ya kwanza atapata viti kadhaa bungeni. Watafanya kila waliwezalo kulemaza juhudi za rais. Hakika Macron atakuwa na kibarua tele.

Kwa kuendeleza kampeni ya kuunga mkono Umoja wa Ulaya, utandawazi na uhamiaji. Vyote ambavyo wenye siasa kali za mrengo wa kulia hawakutaka na akashinda. Hilo pekee ni ufaulu wake. Umoja wa Ulaya unastahili kumsaidia ikiwa inataka kufaulu. Huenda akaweza kuondoa Ufaransa kutoka katika migogoro yake ya kudumu. Lakini hataweza kutimiza hayo peke yake.

Mwandishi: John Juma/DW-English

Mhariri: Josephat Charo

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW