1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chanjo ya mpox kuchukuwa muda mrefu zaidi Kongo

18 Oktoba 2024

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetakiwa kuchukuwa juhudi kubwa za kujenga ufahamu wa watu kuhusu virusi vya mpox na upatikanaji wa chanjo.

Chanjo ya mpox kuchukuwa muda mrefu zaidi Kongo
Chanjo ya mpox kuchukuwa muda mrefu zaidi KongoPicha: Ernest Muhero/DW

Mkuu wa timu ya kukabiliana na mpox nchini humo, Cris Kacita, ameonya kuwa kampeni ya kusambaza chanjo inaweza kuchukuwa muda mrefu kuliko siku kumi zilizotarajiwa mwanzoni.

Kampeni ya chanjo ya mpox nchini Kongo ilizinduliwa mwezi huu katika eneo la mashariki lililoathirika zaidi. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, wakaazi wa jimbo la Kivu Kaskazini kulikoanza kutolewa chanjo hiyo, wanaonekana kutofahamu mengi na wana mashaka nayo.

Kampeni hiyo ya chanjo ni hatua muhimu katika juhudi za kudhibiti mripuko wa ugonjwa huo katika kitovu chake, na ambao sasa umeenea katika mataifa mengine mengi ya Afrika.