1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chanjo ya Urusi dhidi ya COVID-19 yatiliwa shaka

12 Agosti 2020

Wizara ya afya ya Urusi imesema chanjo yake dhidi ya virusi vya corona huenda ikatolewa kwa wahudumu wa afya ndani ya wiki chache zijazo, huku nchi kadhaa ikiwemo Marekani zikiitilia mashaka chanjo hiyo.

Coronavirus | Russland Impfstoff zugelassen
Picha: AFP/Russian Direct Investment Fund

Waziri wa Afya wa Urusi, Mikhail Murashko amesema kwamba chanjo dhidi ya virusi vya corona itatolewa kwanza kwa wataalamu wa afya. Urusi inashikilia nafasi ya nne kuwa na idadi kubwa ya maambukizi ya kirusi hicho kwa kuwa na visa 900,000. Wanasayansi duniani wamekuwa katika mbio za kutengeneza chanjo, lakini tangazo la Urusi la kufanikisha upatikanaje wake, limeibua wasiwasi na mjadala huku wataalamu wakionya kuwa majaribio ya hospitalini yalikuwa yafanyike kwa muda mrefu. Waziri Murashko ameongeza kuwa.

"Wazalishaji walioko ndani ya shirikisho la Urusi watazingatia soko la ndani kwasababu lazima tutimize mahitaji ya raia wetu. Hata hivyo tutatoa chanjo hiyo kwa nchi nyingine na mazungumzo kama hayo yanaendelea. Mfuko wa uwekezaji wa Urusi umejiunga kwenye kazi ya teknolojia na usambazaji. Uzalishaji wa chanjo ya Urusi ya covid-19 katika nchi nyingine unawezekana," alisema Murashko.

Chanjo hiyo imepewa jina la Sputnik, jina la mwanaume wa kwanza kurusha satelaiti katika Orbiti, ikiwa ni mafanikio ya programu ya anga ya enzi za kisovieti miaka ya 1950 dhidi ya hasimu wake Marekani.

Picha ya chanjo iliytolewa na UrusiPicha: AFP/Russian Direct Investment Fund

Waziri wa Afya wa Marekani Alex Azar, ameelezea wasiwasi wake juu ya madai ya Urusi kuwa taifa la kwanza kupata chanjo ya corona, akisema hakuna data za kutosha kuhusu majaribio ya awali. Azar ametoa kauli hiyo Jumatano wakati alipohitimisha ziara yake huko Taiwan. Marekani ni taifa ambalo limeathirika zaidi na janga hilo kwa kuwa na maambukizi karibu milioni 5.1 na vifo zaidi ya 163,000.

Nayo wizara ya afya ya Iran imeonya juu ya matumizi ya chanjo hiyo, ambapo msemaji wake Kianush Jahanpur amesema "kabla ya majaribio yote ya kliniki kukamilika, utumiaji wa chanjo ni kama kutafuta matatizo na kwa hivyo ni hatari". Kama ilivyo kwa nchi nyingine Iran nayo inaifanyia kazi chanjo yake. Israel kwa upande wake imedai kuwa itaitathmini chanjo hiyo na kufanya mazungumzo na Urusi ya kuinunua ikiwa itafaa.

Wakati mataifa mengine yakiitilia shaka, Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte yeye amejitolea kuijaribu chanjo hiyo, wakati taifa likikubali ombi la Urusi la kushiriki kwenye majaribio, usambazaji wa chanjo na uzalishaji wake. Ufilipino yenye watu milioni 107 ina visa vya maambukizi 143,000 ikiwa ni ya pili katika ukanda wa Kusini mashariki mwa Asia baada ya Indonesia na vifo 2,400.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW