MigogoroAfrika
Chanzo: Mazungumzo kati ya DRC na M23 yanaendelea "vyema"
11 Julai 2025
Matangazo
Hayo yameelezwa na mwanadiplomasia wa Qatar kwa sharti la kutotajwa jina akisisitiza kuwa wawakilishi wa pande hizo mbili wanajadiliana kuhusu namna ya kupunguza mateso ya wakazi wa Mashariki mwa Kongo, kuimarisha mpango wa usitishaji mapigano na kuhimiza hatua zaidi kuelekea maridhiano.
Wiki iliyopita, waasi wa M23 walishauri kufanyike mazungumzo zaidi yatakayoshughulikia matatizo ambayo hayakujadiliwa katika makubaliano ya amani kati ya Rwanda na Kongo yaliyotiwa saini mjini Washington mwezi uliopita yakilenga kumaliza mzozo wa miongo kadhaa huko mashariki mwa Kongo.