1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chapisho la Musk kuhusu AfD lawakera wanasiasa wa Ujerumani

21 Desemba 2024

Chapisho la Elon Musk kwenye ukurasa wa X linalodai kuwa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha AfD pekee ndicho kinaweza "kuiokoa Ujerumani" limezua shutuma za kutaka kuingilia uchaguzi ujao nchini humo.

Elon Musk
Elon Musk awakera wanasiasa wa Ujerumani baada ya kuchapisha kwamba chama kinachopinga wahamiaji ndicho kinaweza kuiokoa UjerumaniPicha: Bonnie Cash/Newscom/picture alliance

Bilionea huyo, alichapisha ujumbe huo kwenye video iliyomuhusu kiongozi wa chama cha mrengo wa kulia cha CDU nchini Ujerumani Friedrich Merz.

Serikali ya Ujerumani imejizuia kutoa maoni, lakini wabunge wa pande zote zilizokataa kushirikiana na AfD, walijibu kwa ghadhabu matamshi hayo ya Musk.

Mbunge wa chama cha CDU, Dennis Radtke, alisema inatisha, inakera na haikubaliki kwa mtu muhimu katika serikali ijayo ya Marekani kuingilia kampeni ya uchaguzi wa Ujerumani.

Video hiyo ilimkosoa Merz, anayepewa nafasi kubwa ya kuwa kansela baada ya uchaguzi wa Februari, kufuatia kukataa kushirikiana na chama hicho cha AfD kinachopinga wahamiaji, ambacho kwa sasa kinashikilia nafasi ya pili.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW