1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chapo afuta ziara yake ya Davos kutokana na mafuriko

19 Januari 2026

Rais wa Msumbiji Daniel Chapo amefuta ziara yake ya kuelekea Davos kuhudhuria Kongamano la Kiuchumi la Dunia nchini Uswisi wiki hii, kutokana na mafuriko ambayo yameathiri mamia ya maelfu ya watu nchini mwake.

Msumbiji Maputo 2025 | Rais Daniel Chapo
Rais wa Msumbiji Daniel Chapo wakati wa hafla ya kuapishwa kwake mnamo Januari 15, 2025Picha: Carlos Uqueio/AP Photo/picture alliance

Katika chapisho kwenye mtandao wa Facebook hapo jana, Chapo amesema Msumbiji inapitia wakati mgumu na kipaumbele kwa wakati huu ni kuokoa maisha.

Mvua kubwa iliyonyesha tangu katikati ya Desemba imesababisha mafuriko makubwa

katika mikoa ya Gaza, Maputo na Sofala nchini humo, huku mabonde ya mito yakiongeza maji yake kufikia viwango vya kutisha.

Haya ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa jana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu, OCHA.

OCHA imesema mamlaka imekadiria kuwa zaidi ya watu 400,000 wameathirika, huku idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka katika wakati ambapo mvua inaendelea kunyesha.

Mvua kubwa pia imeathiri maeneo ya Afrika Kusini, ikiwa ni pamoja na kaskazini mashariki ilipo mbuga yake ya kitaifa ya Kruger .

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW