EU:Ni sharti Urusi iache mzingiro wake wa bandari za Ukraine
8 Septemba 2023Akizungumza na waandishi habari mjini New Delhi India kuelekea mkutano wa kilele wa G20, Michel amesisitiza kuwa meli zenye nafaka zinahitaji kupita salama kwenye Bahari Nyeusi na kwamba mpango wa Umoja wa Mataifa umefikisha tani 3232 kwenye masoko hususan katika mataifa maskini. Aidha Michel amesema:
"Zaidi ya watu milioni 250 wanakabiliwa na uhaba wa chakula duniani kote, na kwa kushambulia kwa makusudi msaada wa Ukraine, Kremlin inawanyima chakula wanachohitaji sana. Kwa kweli ni kashfa kwamba Urusi, baada ya kusitisha Mpango wa kusafirisha nafaka kupitia Bahari Nyeusi, inazuia na kushambulia bandari za Ukraine. Hii lazima ikome.”
Urusi ilijitoa kwenye makubaliano hayo mwezi Julai ikidai ulishindwa kutimiza lengo la kuondoa njaa barani Afrika.
Urusi imeiomba Uturuki kuisaidia kusafirisha nafaka zake kuelekea Afrika bila ya kuihusisha Ukraine.