1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chelsea mkono mmoja kwenye taji la Premier Uingereza

27 Aprili 2015

Taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya Premier Uingereza linaweza kuwa tayari limeshaingia kapuni kwa Chelsea iwapo siku ya Jumatano mabingwa hao watarajiwa watafanikiwa kuishinda Leicester City.

Fußballer Diego Costa und Eden Hazard (FC Chelsea)
Picha: picture-alliance/dpa/F. Arrizabalaga

Ushindi mara nne mfululizo umeiwezesha Leicester kujitoa kutoka katika eneo la hatari ya kushuka daraja , na wakati Hull City ambayo nayo inatapia kujinasua kutoka hatari ya kushuka daraja inapambana na Liverpool kesho Jumanne, taswira ya nani atatumbukia katika mzozo mwingine wa kushuka daraja itaweza kuwa wazi kiasi. Kutawazwa kwa Chelsea kama mabingwa wa Premier League kunaonekana kuwa na uhakika lakini inabidi timu hiyo ijihadhari na kikosi hicho ambacho kiko katika hali bora hivi sasa. "tuko karibu na ubingwa lakini tuna mchezo mgumu Jumatano dhidi ya Leicester," amesema nahodha John Terry.

Wakati huo Eden Hazard ameteuliwa na wachezaji wa ligi ya Uingereza kunyakua taji la mchezaji wa mwaka nchini Uingereza kutokana na ustadi wake wa kusakata kandanda uwanjani.

Eden Hazard ndiye mchezeji bora wa mwaka katika ligi kuu ya Premier - UingerezaPicha: Reuters/Andrew Winning

Winga huyo Mbelgiji mwenye umri wa miaka 24 alipata taji la mchezaji chipukizi mwaka jana na sasa ni mchezaji bora wa mwaka , na taji lake hilo la mwaka jana limechukuliwa na mshambuliaji wa Tottenham Hot Spurs Harry Kane.

Kocha Louis van Gaal amesema Manchester United imeiweka Liverpool katika kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya kucheza katika Champions League mwakani baada ya kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Everton jana Jumapili. Liverpool iko nyuma ya Manchester kwa pointi 7 lakini ina mchezo mmoja kibindoni bado na itacheza michezo yake miwili kabla ya mchezo mwingine wa Manchester, dhidi ya West Bromwich Albion , ikiwa na maana huenda kikosi cha van Gaal kikawa na pointi moja tu ya ziada wakati itakapoingia uwanjani kwa mchezo wake mwingine.

Real Madrid inawania kufanya mbapambano wa kuwania ubingwa wa Ligi ya Uhispania , La Liga kuamuliwa dakika za mwisho, kwa kuishinda Almeria siku ya Jumatano na kisha kushinda michezo yake minne ya mwisho.

Real inawania kuweka mbinyo kwa Barca kwa kuishinda Almeria iliyoko mkiani siku ya Jumatano.

Mkakati wetu ni kuwanyima Barca fursa ya kushinda kila kitu msimu huu. Tarakimu hazitupi hali mbadala wa mkakati huu," kocha wa Real Carlo Ancelotti amesema baada ya ushindi wa mabao 4-2 wa timu yake dhidi ya Selta Vigo jana Jumapili.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / ape / rtre
Mhariri: Yusuf , Saumu

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW