1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chelsea mkono mmoja kwenye taji la Premier

20 Aprili 2015

Kule Uingereza, Chelsea wanahitaji tu ushindi wa mechi mbili zijazo na kutwaa ubingwa wa Ligi ya Premier, baada ya ushindi wa goli moja kwa sifuri dhidi ya Manchester United.

England, FC Chelsea - Manchester City
Picha: picture-alliance/dpa/EPA/F. Arrizabalaga

Uhindi huo dhidi ya nambari tatu, umewaweka vijana hao wa Jose Mourinho kileleni mwa ligi kuu ya Premier na pengo la pointi kumi.

Chelsea ambao wana pointi 76 kutokana na mechi 32, wanaweza kutwaa ubingwa kama wataipiga Arsenal, wikendi ijayo na kisha kushinda mchuano wao wa ziada dhidi ya Leicester City.

United wanasalia katika nafasi ya tatu na pointi 65 huku mahasimu wao Manchester City wakiwa nyuma yao na pengo la pointi moja baada ya kupata ushindi wa mbili bila dhidi ya West Ham United.

Katika Kombe la FA, sasa ni wazi kwamba Arsenal itapambana na Aston Villa katika fainali ya dimba hilo itakayoandaliwa Wembley Mei 30. Villa waliwaduwaza Liverpool kwa ushindi wa mabao mawili kwa moja wakati Arsenal ikipambana na kupata ushindi kama huo dhidi ya Reading.

Nchini Uhispania, Lionel Messi aliwafungia viongozi wa La Liga, Barcelona, goli lake la 400 na kuwapa ushindi wa 2 - 0 dhidi ya Valencia. Ushindi huo umewaweka mbele ya Real Madrid na pengo la pointi mbili hata baada ya wapinzano hao kuwazaba Malaga mabao matatu kwa moja dhidi ya Malaga. Nayo Atletico Madrid ilipata ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Deportivo la Coruna na kuwaweka katika nafasi ya tatu na pengo la pointi nne dhidi ya nambari nne.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Yusuf Saumu

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW