1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChile

Chile yaunga mkono kesi dhidi ya Israel huko ICJ

2 Juni 2024

Rais wa Chile Gabriel Boric amesema nchi yake inaungana na Afrika Kusini dhidi ya Israel katika kesi yake katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ.

Rais wa Chile Gabriel Boric
Rais wa Chile Gabriel Boric Picha: Rodrigo Garrido/REUTERS

Akihutubia bunge la nchi yake Jumamosi (01.06.2024), Boric alishutumu hali mbaya ya kibinadamu huko Gaza na kutoa wito wa majibu madhubuti kutoka kwa jumuiya ya kimataifa.

Rais wa Chile amesema nchi yake itakuwa mshiriki na kuunga mkono kesi ambayo Afrika Kusini iliwasilisha dhidi ya Israel mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki huko The Hague.

Mahakama ya ICJ inazingatia kesi ya Afrika Kusini, lakini kwa muda mfupi imetoa uamuzi wa awali kuiamuru Israeli kufanya kila iwezalo kuzuia vitendo vya mauaji ya halaiki wakati wa operesheni yake dhidi ya Hamas.

Nchi ya Chile imeitambua Palestina kama taifa tangu mwaka 2011, na rais Gabriel Boric alishawahi kusema kuwa vita vya Gaza "havina uhalali" na "havikubaliki."

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW