1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMalawi

Chilima kupewa heshima ya mazishi ya kitaifa nchini Malawi

12 Juni 2024

Serikali ya Malawi imesema jumatano 12.06.2024 kuwa Makamu wa Rais Saulos Chilima atapewa heshima ya mazishi ya kitaifa baada ya kufariki katika ajali ya ndege pamoja na watu wengine wanane.

Miili ya waliopoteza maisha yao kufuatia ajali ya ndege Malawi
Miili ya waliopoteza maisha yao kufuatia ajali ya ndege MalawiPicha: Zambia Air Force via REUTERS

Katika taarifa, Rais Lazarus Chakwera ameteuwa kamati ya mawaziri kusimamia maandalizi ya mazishi hayo ya kitaifa ya Chilima.

Rais Chakwera alikuwa tayari ameshatangaza siku 21 za maombolezo ya kitaifa jana, mabaki ya ndege iliyokuwa imembeba makamu huyo wa rais na wenzake yalipopatikana katika eneo moja la milimani kaskazini mwa nchi hiyo.

Bendera zitapepea nusu mlingoti kote nchini humo katika kipindi hicho cha maombolezo.

Awali rais huyo alikuwa ametangaza kwamba watu 10 ndio waliokuwa ndani ya ndege hiyo ila serikali sasa inasema kwamba ni watu tisa waliokuwemo wakati ajali hiyo ilipotokea.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW