1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China: Hatutaruhusu Taiwan ijitawale kamwe

10 Aprili 2026

China imesema haitaruhusu Taiwan ijitawale hatua iliyotajwa na Rais Xi Jinping ndio chanzo cha kudhoofika kwa amani katika Mlango wa Bahari wa Taiwan. Rais Xi amesema hayo alipokutana na kiongozi wa upinzani Taiwan.

China, Beijing 2026 | Xi Jinping na  Cheng Li-wun
Rais wa China Xi Jinping akiwa na Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Taiwan KMT Cheng Li-wun Picha: Xie Huanchi/Xinhua/IMAGO

Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Taiwan cha KMT Cheng Li-wun anafanya ziara hiyo nchini China baada ya kipindi cha takriban miaka kumi kupita, ziara ikilenga kupunguza mvutano wakati ambapo Beijing ikiongeza shinikizo la kijeshi dhidi ya kisiwa hicho ambacho inakichukulia kama sehemu ya himaya yake. 

Katika mkutano huo uliovuta nadhari ya kikanda Rais Xi alimwambia Cheng kuwa dunia ya leo iliyogubikwa na mizozo kuchagua amani ni jambo muhimu na lenye thamani kubwa.

Rais Xi pia aligusia suala nyeti la muungano kati ya China na Taiwan, ambalo kwa muda mrefu limekuwa lengo la Beijing, linapingwa vikali na serikali ya Taiwan.

"Mkutano huu kati ya viongozi wa vyama viwili unalenga kulinda amani na utulivu wa nchi yetu ya pamoja, na kukuza maendeleo ya amani ya uhusiano wa Mlango Bahari wa Taiwan," Alisema Rais Xi.

Aliongeza kuwa mazungumzo hayo ya pande mbili yanalenga kuweka mustakabali bora kwa vizazi vijavyo, kwa kujenga msingi bora wa kisiasa na kuzingatia makubaliano ya mwaka 1992 na kupinga uhuru wa Taiwan.

"Tutashirikiana na vyama mbalimbali vya kisiasa na makundi yote Taiwan ili kuimarisha mawiliano na mazungumzo."

Ikumbukwe kwamba China imekuwa ikikwepa kufanya mazungumzo na Rais wa Taiwan Lai Ching-te ikimshutumu kuendeleza sera za kujitenga.

Taiwan: China inapaswa kuzungumza na serikali iliyochaguliwa 

Serikali ya Taipei imemtaka Cheng kuiambia Beijing kuwa iachane na vitisho vyake dhidi ya Taiwan na kwamba inapaswa kushirikiana  na serikali iliyochaguliwa kidemokrasia.

Kwa upande wake Cheng amemwambia rais Xi kuwa Taiwan kamwe haitakuwa kitovu cha kuchochea migogoro na nguvu kutoka nje.

Kiongozi wa chama cha upinzani Taiwan cha KMT Cheng Li-wunPicha: Tingshu Wang/REUTERS

"Taiwan haitakuwa tena kitovu cha uwezekano wa mivutano, wala wala haitageuzwa kuwa chombo cha kuchezewa na nguvu kutoka nje. Taiiwan itakuwa njioa yakuunganisha udugu, ustaarabu na matumaini."

Chama cha kikomunisti cha KMT kiliwahi kuitawala China hadi mwaka 1949 kabla ya kufurushwa hadi Taiwan ilipo shindwa vita vya wenyewe kwa wenyewe dhidi ya vuguvugu la kikomunisti la Mao Zedong, lililounda jamhuri ya watu wa China.

Hakujawahi kusainiwa mkataba wa amani wala makubaliano ya kusitisha mapigano, na hadi sasa, hakuna kati ya serikali hizo mbili inayotambua rasmi uhalali wa mwenzake.

Wakati mvutano ukizidi kuongezeka baina ya China na Taiwan, Marekani imekuwa ikijipambanua kama mshirika mkuu wa kimataifa wa Taipei na ndiyo msambazaji muhimu wa silaha licha ya kutokuwapo kwa uhusiano rasmi wa kidiplomasia kati yao. Beijing imekuwa ikiitaka mara kwa mara Washington iache kuipatia Taipei silaha. 

Nancy Pelosi awasili Taiwan

01:24

This browser does not support the video element.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW