1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Jinping: Uchumi waimarika, aahidi kuungana tena na Taiwan

31 Desemba 2023

Rais Xi Jinping amesema kwamba uchumi wa China kwa mwaka 2023 uliimarika na kuwa wenye ustahimilivu na nguvu zaidi licha ya mawimbi yaliyoshuhudiwa.

China Xi Jinping akihutoa hotuba ya mwaka mpya
Rais wa China Xi Jinping akitoa hotuba muhimu ya mwaka mpya mbele ya hadhara Disemba 29, 2023Picha: Yao Dawei/Xinhua News Agency/picture alliance

 Xi Jinping anasema hayo licha ya ripoti za kifedha kuendelea kuwa mbaya huku ukuaji wake katika kipindi cha baada ya janga la UVIKO-19 ukijikongoja.

Xi aidha kwa mara nyingine ameahidi kwenye hotuba hiyo kwa taifa kwamba China itaungana tena na Taiwan ambayo China inadai kuwa ni himaya yake.

China imepitia changamoto kwa mwaka 2023, likiwa taifa la pili kwa uchumi mkubwa ulimwenguni, huku serikali ikipambana kuendeleza hatua za kuimarisha uchumi wake tangu ilipoachana na sera yake ngumu ya kukabiliana na UVIKO-19 mwaka uliopita.

Xi ameahidi mwaka ujao kuunganisha na kuimarisha mwelekeo chanya wa kufufua uchumi na kufikia utulivu wa kiuchumi wa muda mrefu.